SEMINA KUHUSU KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO NA MFUMO WAKE[1] KANISA LA TEGETA SDA TAREHE 6 APR 2013
1.
UTANGULIZI
·
Agizo la injili la
Mwokozi wetu Yesu Kristo la kupeleka injili ulimwenguni kote ni kazi yenye
utisho (Math 28:19, 20). Madhehebu yote yanakubali kwa kiasi fulani wajibu huu.
Lakini Waadventista Wasabato wanasimama peke yao katika kujisikia kuwajibika
katika kupeleka ujumbe wa malaika wa tatu “kwa kila taifa, kabila, lugha
na jamaa”
(Uf. 14:6).
·
Hivyo, mfumo wa kanisa ni
wa lazima katika kutekeleza agizo hilo.
·
Kanisa mahalia lolote
lile linalolenga katika shughuli mahalia tu limepoteza njozi ya pekee ya kanisa
la waadventista Wasabato kiulimwengu (Mwongozo wa Wazee, 2007 Uk. 22; Kazi ya
sadaka za kila robo – Angalia “Lesson ya watu wazima, Robo II, 2013).
·
Waadventista Wasabato
wanaamini kwamba kazi haitamalizika popote mpaka
imalizike kote.
·
Mtazamo wa kanisa kiulimwengu
huleta changamoto kubwa ya kimfumo, hivyo:
Ø Hainabudi
mfumo wa kanisa ieleweke kwa kila
muumini kanisani.
Ø Mfumo
lazima uwe wa ufanisi.
Ø
Kazi ni ya kiulimwengu
mzima hivyo lazima yawepo mamlaka ya kutosha yaliyobainishwa kwa ngazi za
utawala nje ya kanisa mahalia ili kuwe na uhakika wa
mgawanyo wa ulinganifu wa watendakazi na pesa;
Ø
Kazi ni ya mataifa
mengi na tamaduni nyingi hivyo mfumo haunabudi kuwa unaoweza kubadilika kirahisi kupokea mazingira mapya (flexible) (Uf 14:6).
2.
HISTORIA
YA MWANZO WA WAADVENTISTA WA SABATO
·
Historia ya mwanzo wa Waadventista
inaanzia kwa mhubiri mashuhuri William Miller (1782).
·
Miller alikuwa Mkristo
Mbaptisti, lakini hakuridhika na kanisa lake, kwa kutojibu maswali yake mengi
yaliyokuwa yanamsumbua.
·
Mwaka 1816 (akiwa na
miaka 34 tu) alianza kusoma na kuchunguza Biblia kwa dhati.
·
Katika usomaji huo alitafsiri
Dan 8:14 na kufikia uamuzi kuwa Yesu angerudi tarehe 22 Oktoba 1844.
·
Miller alianza kuhubiri
kwa nguvu juu ya kurudi kwa Yesu mara ya pili 14 Agosti 1831. Aliendelea
kuhubiri kwa miaka 13 (www.sdaisrael.org
– Our Identity).
Ø Alitoa
mahubiri 4,000 katika miji 500.
Ø Zaidi
ya wachungaji (clergy) 200 walimwamini.
Ø Watu
wapatao 100,000 waliamua kumfuata na waliitwa “Millerites”.
·
Siku hiyo ilipofika na
Yesu hakuja ilikuwa ni siku ya huzuni kubwa (“Great Disappointment.”)
·
Wale waliosalia baada
ya kukatishwa tamaa kikuu waligawanyika katika makundi mawili:
Ø Wengine
waliamini kuwa tukio la kurudi kwa Yesu lilikuwa sahihi ila tarehe ilikosewa,
hivyo wakaanza kupanga tarehe zingine.
Ø Kundi
la pili walielewa kuwa Masihi angekuja haraka, kwamba wakati walitafsiri tukio
vibaya, lakini tarehe ilikuwa sahihi. Walikataa kuweka tarehe nyingine mpya, na
kugeukia Neno la Mungu, waliendelea kuchunguza ukweli wa Biblia kwa bidii.
Waadventista Wasabato wametokana na kundi
hili la pili.
·
Kadiri walivyoendelea
kutafuta ukweli wa Biblia waligundua (rediscovered) ukweli wa sabato.
·
Wakati huo huo, Hiram
Edson, mkulima mmoja (local farmer) huko Marekani, katika kujifunza Biblia alikuja
kuelewa wapi William Miller alikosea katika kutafsiri patakatifu. Aligundua
kuwa kulingana na Biblia, patakatifu pa duniani ilikuwa mfano tu wa patakatifu
pa mbinguni (Kut. 25:9).
·
Maendeleo baada ya siku
ya huzuni kubwa “Great Disappointment”:
1844-1863:
Ø Joseph
Bates na James White na Ellen White walisafiri kote katika New England wakiendesha
madarasa ya Biblia, kuunda vikundi vya maombi, na kujenga umoja wa Mafundisho Makuu. Mama White alichangia
kiasi kikubwa katika kazi hii.
Ø Matokeo
ya kazi yao ilizaa pamoja na mambo mengine: Utunzaji wa Sabato; Utunzaji wa miili
yetu; na Kuishi kiafya na Imani katika kupeleka Injili.
|
1863
na kuendelea:
Ø Mwaka
1863 Kanisa la Waadventista Wasabato liliundwa rasmi likiwa na waumini 3,500.
Ø Makao
Makuu ya Kanisa yalikuwa Battle Creek, Michigan Marekani (sasa yako Silver Spring
Maryland, Marekani).
Ø Mwaka
1900 waumini walimuwa 75,000; 1955 waumini zaidi ya waumini 1,000,000. Leo
kanisa lina waumini wapatao milioni 20 duniani kote.
|
·
Mwaka huu, 2013 Kanisa
la Waadventista Wasabato linatimiza miaka 150 tangu lianzishwe rasmi mwaka 1863
huko Marekani.
·
Sherehe za miaka 150
zitafanyika katika makanisa yote kote duniani. Mipango ya namna makanisa yatakavyofanya sherehe hizo imeachwa
kwa makanisa husika yenyewe au katika mitaa
yao, katika Konferensi au katika Union husika. Mambo muhimu yanayotiliwa
mkazo katika sherehe hizo ni:
Ø Kujikita
katika Mafundisho Makuu ya Imani
Ø Uinjilist
(Evangelism).
Ø Utunzaji (Nurturing & Retention).
Ø Kujumuika
kama Familia ya Mungu (Fellowship)
3.
AINA
YA MFUMO NA UTAWALA WA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO
·
Kuna aina 4 za utawala
wa kanisa
Na.
|
Aina ya
Utawala
|
Mfumo wa
Utawala
|
Mfano wa
Kanisa
|
|
|
|
|
1.
|
Utawala wa Kipapa
|
Ambapo Papa ana mamlaka ya juu kabisa
|
Katoliki
|
2.
|
Utawala wa Kiaskofu
|
Mamlaka ya mwisho yapo kwa maaskofu wa
kanisa
|
Lutheran & Anglican
|
3.
|
Utawala wa Kujitegemea
|
Mamlaka kamili ndani ya milki ya
kanisa yapo kwenye kusanyiko mahalia
|
Makanisa ya Kipendekosti
|
4.
|
Utawala wa Kiuwakilishi
|
Mamlaka yapo kwa washiriki wa kanisa,
lakini wajibu wa kupanga na kuratibu umeanishwa kwa ngazi nyingine.
|
Waadventista Wasabato
|
·
Kanisa la Waadventista
Wasabato hufuata mfumo wa kiuwakilishi (ambapo kura ya wengi) katika utawala
wake.
·
Si lazima watu wote
wapige kura, maamuzi yanafanyika kwa wingi wa idadi ya watu waliopiga kura
·
Kazi ya kila ngazi ya Kanisa
la Waadventista Wasabato hutathminiwa katika kila Sesheni (sessions) za kimihula (Kanisa Mahalia kila mwaka,
Konferensi/Union/GC kila baada ya miaka mitano).
·
Katika Sesheni hizi taarifa zinatolewa,
viongozi wanawajibishwa na uongozi mpya unachaguliwa.
·
Wajumbe wa sesheni hizi wanachaguliwa hasa na ngazi
iliyo chini ya ile inayotathminiwa. Kwa mfano, kabla ya sesheni ya Konferensi mahalia kila kanisa wanachagua wajumbe kutoka
katika waumini wake kuliwakilisha katika sesheni.
·
Awali wakati kanisa lilipoanza
hapakuwepo na mfumo wo wote. Lakini kadri waumini na shughuli za kanisa
zilipoendelea kuongezeka kukawa na haja ya kuwa na mfumo wa kanisa kwa sababu
kuu zifuatazo:
Ø
Ili kuhifadhi na
kumiliki mali za kanisa.
Ø
Ili kutambulisha yupi
ni mchungaji wa kanisa letu wetu na yupi siye.
Ø
Ili kulipa wachungaji.
4.
MADARAJA
YA MFUMO WA UTAWALA WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO
|
Mfumo
wa Kawaida (Standard Design)
|
|
Mfumo
Mbadala (Alternative Design)
|
1.
|
Kanisa Mahalia (Local
Church)
|
1.
|
Kanisa Mahalia (Local
Chrch)
|
2.
|
Konferensi Misheni (Conf. Mission)
|
2.
|
Union of Churches
|
3.
|
Union
Conference/Mission
|
3.
|
Division
|
4.
|
Division
|
4.
|
General Conference
|
5.
|
General Conference
|
|
|
5.
USHIRIKA
(MEMBERSHIP)
Kanisa Mahalia
|
Watu
|
Konferensi Mahalia
|
Makanisa
|
Union
|
Ma-Konferensi
|
General Conference
|
Unions
Conferences/Mission
|
1)
Ushirika
Unapatikanaji
a.
Mtu hawezi kuwa
mshiriki kwa mwenyewe, lazima kundi moja la watu wakufanye kuwa mshiriki. Ushirika ni haki/dhamana unayopewa na kanisa siyo mali yako. Unaweza
kupewa na unaweza kunyang’anywa.
b. Mtu
hawezi kujibatiza mwenyewe, lazima ubatizwe na kundi Fulani ya watu.
c. Ushirika
kwa kanisa ni kwa njia moja tu kwa KURA.
2)
Mamlaka/Madaraka
a. Katika
Kanisa la Waadventista Wasabato mamlaka ya mwisho haikuachwa juu ya KUNDI (group) moja tu la waumini wala kwa MTU MMOJA au KIKUNDI KIMOJA pekee yake.
b. Mamlaka
ya KUNDI la watu daima yako juu kuliko mamlaka ya mtu mmoja.
c. MAMLAKA YA MWISHO
(FINAL authority) haikuwekwa katika SEHEMU
MOJA TU. Kila ngazi ya mamlaka ina baadhi tu ya madaraka.
Na.
|
Daraja la
Utawala
|
Majukumu
|
|
|
|
1.
|
Kanisa Mahalia
|
-
Haina mamlaka yote bali baadhi tu.
-
Ina mamlaka ya mwisho tu juu ya
ushirika wa mtu: nani awe mshiriki na
nani asiwe mshiriki (ndiyo MAMLAKA YA MWISHO peke yake iliyonayo).
|
2.
|
Konferensi/Fildi/Misheni
|
-
Konferensi haina mamlaka yote bali
baadhi tu.
-
Ina mamlaka ya mwisho tu juu ya Kupanga
na kuondoa makanisa
|
3.
|
Union
-
Union inayojitegemea
[union conference]
-
Union Misheni [union
tegemezi], n.k.
|
-
Union haina mamlaka yote bali baadhi
tu.
-
Ina mamlaka ya mwisho tu juu ya
Kupanga na kuondoa ma-konferensi
|
4.
|
Halmashauri Kuu [general conference]
|
-
GC haina mamlaka yote bali baadhi tu.
-
Ina mamlaka ya MWISHO
juu ya Misingi ya Imani na Kanuni za Kanisa
|
3)
Mamlaka
ya kila ngazi na Athari (Impact) zake
·
Maamuzi yo yote magumu ya
Kanisa mahalia yataadhiri àmoja
kwa moja washiriki (watu) wa kanisa hilo tu. Mathalan,
kufutwa ushirika n.k.
·
Maamuzi magumu ya Konferensi yataathiri àutendaji
wa kanisa mahalia moja kwa moja. Hatua hiyo hatimaye
yataathiri àwashiriki
pia. Mathalan – kupewa karipio au kufutwa kwa kanisa.
·
Maamuzi magumu ya Union yataathiri àKonferensi
mahalia na kwenda chini kwa àmakanisa yake
na kwenda chini zaidi kwa àwashiriki
wake. Mathalan kufutwa kwa Konferensi.
·
Maamuzi magumu ya GC yataathiri moja kwa moja àUnion husika na kwenda chini
kwa àMa-konferensi
na chini zaidi kwa àmakanisa
ya konferensi hiyo na mwisho kabisa kwa àwashiriki. Kwa mfano
kufutwa kwa Union.
Hivyo
basi, mfumo wa kanisa la Waadventista Wasabato hatimaye hugusa kila mshiriki
kwa hatua za maamuzi magumu.
6.
TAKWIMU
ZA GC KUFIKIA JULAI 2012
a. Total
Members - >17
million
b. Local
churches - 71,000
c. Companies - 65,000
d. Local
Conferences - 321
e. Local
Mission - 264
f. Union
Conferences - 51
g. Conference
Mission - 55
h. Union of
Churches - 13?????
i. Division - 13
j. GC - 1
k. Countries
with SDA presence - 209
IMETAYARISHWA NA:
Damba Omara
Mzee wa Kanisa
VIANZO REJEA: Kanuni za Kanisa Toleo la
17; Mwongozo
wa Wazee – Kanisa na Mfumo Wake uk. 12-24; Semina ya Wachungaji na Wazee wa
Kanisa, Morogoro, 24-27 Jani 2013; na www.sdaisrael.org – Our Identity).
Post a Comment