MATANGAZO YA KANISA 13/04/2013
1.
Tunamshukuru sana Mungu kwa kutulinda kwa wiki nzima hadi Sabato ya leo.
Tunawakaribisha wageni kwa wenyeji katika Ibada ya leo.
2. Mkuu wa idara ya watoto (Mama Maingu)
anaomba kukutana na wafuatao saa 10 leo jioni; mzee wa idara ya watoto, walimu
wpte wa watoto, mkuu wa S.S. watoto,
viongozi wa VBS, PF na AC. Ni muhimu sana.
3. Semina ya Kulea
na Kutunza Washiriki itafanyika kanisani Ilala tarehe 13-14/04/2013. Siku
ya J’Mosi tar 13 watakaohudhuria ni:
Wachungaji, Wazee wa Kanisa, Karani wa Kanisa, Mhazini wa Kanisa, Wakuu wa
Huduma na Mashemasi Wakuu kuanzia saa 8 mchana. Siku ya J’Pili tar 14 Wajumbe wote wa Kanisa wahudhurie kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8
mchana.
--baraza la kanisa lilopangwa kufanyika kesho, litafanyika jumapili
ijayo, wakuu wa idara andaeni mipango na taarifa za kazi.
4.
Makambi ya mtaa yanaanza 21-27/07/2013; tutoe michango yetu (50,000/) kwa njia
ya bahasha, muda unaisha.
5. Kamati ya Majengo Mtaa itakutana Tegeta kanisani siku ya sabato tarehe
20/04/2013 saa 11 jioni. Wajumbe wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.
6. Sadaka maalum ya kusaidia uanzishwaji wa Runinga
(TV) ya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania, Inaendelea kukusanywa
tunahimizwa kila mtu achangie angalau Sh. 10,000/- goli la kanisa letu ni Sh.
3,300,000/-,bado hatujalifikia. Runinga itazinduliwa Juni, 2013.
7. Sensa ya washiriki
ili kubainisha washiriki waliopo na wasiokuwepo itafanyika mwisho April 2013.
Toeni ushirikiano wa kutosha kwa kamati hiyo ili kufanikisha zoezi hilo.
8. Sabato maalum kuchangia ujenzi wa nyumba ya mchungaji itafanyika tarehe 04/05/2013 kanisani Tegeta. Mnenaji mkuu
anategemewa kuwa Pr. Toto Bwire Kusaga kutoka ETC. Goli letu ni kukusanya fedha
si chini ya Milioni Ishirini (Tshs 20,000,000/=). Tunahimiza kila kanisa
lijiandae vyema kwa tukio hilo muhimu.
9. Mahubiri
katika Miji Mikuu yataanza
Dodoma tarehe 13 – 28/04/2013.
Kanisa la Tegeta tunatakiwa kuchangia (330,000/-). Tuyaombee na kukamisha
michango yetu.
10.Sabato maalum ya wageni itakuwa ni 13/04/2013,
washiriki tuchangie gharama na kushiriki kualika wageni kwa ajili ya sabato hii
muhimu.
11.
Katika ubao wa matangazo, kuna
mapendekezo ya:
o MAPENDEKEZO YA BAJETI YA KANISA, 2013
o MAPENDEKEZO YA MPANGO MKAKATI WA KANISA
o TAARIFA YA IDARA YA HUDUMA, ROBO YA KWANZA, 2013,
Tunaomba washiriki muisome na kuipitia, kama
kuna mapendekezo ya mabadiliko au
nyongeza yaletwe kwa wazee wa kanisa kwa kupitiwa.
12. Semina ya idara zifiatazo:
shule ya sabato, watoto na wanawake, imeanza shule ya sekondari Kitungwa
Morogoro, 3—6/4/2013, Wakuu wa idara husika wamesharudi.
13. Baraza la Mtaa maalum litakaa tarehe 28/04/2013 kanisani Tegeta saa 3
asubuhi hadi saa 7 kamili mchana. Kikao hiki ni kwa ajili ya Mchungaji, Wazee
wa Kanisa na Makarani wa Kanisa. Tafadhali zingatieni.
14. Maombi ya Jumatano asubuhi yanaendelea saa 11:00
asubuhi, na jioni tunawaalika wote kushiriki.
15. Tanzia:--
--Familia yam zee Kefas Lisso, wamefiwa, shemeji
yake Kefas Lisso, Ukonga, wamesafirisha
Musoma kwa mazishi.
--Familia ya Fred Maiga wamefiwa, mama mkubwa wa
Fred Maiga, wamesafiri Musoma kwa mazishi.
--Familia ya mshiriki wetu, Ndugu Alex Mafuru w amefiwa na shemeji yake Professor Michael Wambali, msiba uko kwake
Wambali Mbweni, Tuwaombee na kuwafariji.
--tuwaombee wafiwa na kuwatembelea kuwafariji.
16. Familia ya Shemasi Joel Nikombolwe wameibiwa gari, Joel alitekwa na majambazi njiani, na kuibiwa gari, tuwaombee na kuwatembelea.
--tuwaombee wafiwa na kuwatembelea kuwafariji.
16. Familia ya Shemasi Joel Nikombolwe wameibiwa gari, Joel alitekwa na majambazi njiani, na kuibiwa gari, tuwaombee na kuwatembelea.
16. Ndoa: (Mara ya Pili)
--Mussa Wilson Sango (Tegeta SDA) na Agape Denis
Bhoke (Kijenge SDA-Arusha), itafungwa 05/05/2013, Mwenge SDA Church.
--Edger Emir Kapallah (Tegeta SDA) na Judith George
Mabula (Mwanza), itafungwa 27/04/2013, Tegeta SDA Church.
--Julius Jackson Nywage (Tegeta SDA) na Dina George
Haule (Luhanga SDA-Iringa), itafungwa, 28/04/2013, Mwenge SDA Church.
17. Mibaraka ya watoto:
--Mke wa mzee wa kanisa R.Barikesha amejifungua kwa
operation, tuwatembelee na kuwaombea.
--Mke wa Bahati Malima alijifungua mtoto kwa
operation, tuwatembelee na kuwaombea.
--Odilia Leornard amejifungua mtoto kwa operation, tumtembelee na kumuombea.
--Odilia Leornard amejifungua mtoto kwa operation, tumtembelee na kumuombea.
18. Jumamosi ya 13/04/2013 ni sabato ya wageni, karibuni wageni wetu na Mungu aaawabariki, tunaposhiriki mibaraka hii.
19.. Zamu:--mzee wa zamu: Joseph Msuya
19.. Zamu:--mzee wa zamu: Joseph Msuya
--shemasi mkuu wa zamu: Eliya Kenani
20.
Utaratibu wa Sabato ya leo—Tarehe 13.04.2013
TUKIO
|
TEGETA
|
WATOTO
|
Mhubiri
|
Mch.
MDAMBI
|
ADAM MSAKU
|
Mwenyekiti
|
MZEE DAMBA OMARA
|
|
Fungu
Kuu na Ombi
|
Mwinj. DICKSON MIPAWA
|
|
Sadaka
& zaka
|
MZEE JOSEPH MSUYA
|
|
Kufunga
Sabato
|
MZEE S.I.M. KAPAYA
|
21.
Utaratibu wa Sabato ijayo—Tarehe 21.04.2013
TUKIO
|
TEGETA
|
WATOTO
|
Mhubiri
|
MZEE
S.I.M.KAPAYA
|
MAMA MAINGU
|
Mwenyekiti
|
MZEE DAMBA OMARA
|
|
Ombi na Fungu Kuu
|
MZEE ERAGA MJULI
|
|
Sadaka/Zaka
|
MZEE R.BARIKESHA
|
|
Maombi J5 (Asb.+Jioni)
|
MZEE JOSEPH
MSUYA
|
|
Kufungua Sabato
|
MZEE
S.I.M.KAPAYA
|
Post a Comment