MATANGAZO YA KANISA 20/04/2013
1.
Tunamshukuru sana Mungu kwa kutulinda kwa wiki nzima hadi Sabato ya leo.
Tunawakaribisha wageni kwa wenyeji katika Ibada ya leo.
2. Sabato maalum ya wageni ilifanyika
13/04/2013, washiriki tunawashukuru kwa kuchangia gharama na kushiriki kualika
wageni kwa ajili ya sabato hii muhimu. Mungu awabariki sana, tuendeleze moyo
huu..
3. Mahubiri katika Miji
Mikuu yameshaanza Dodoma tarehe 13 –
28/04/2013. Tunashukuru kwa michango yenu tuendelee kuyaombea mahubiri
haya.
4. Semina ya Kulea na Kutunza Washiriki ilifanyika
kanisani Ilala tarehe 13-14/04/2013. Baraza la kanisa lilihudhuria.
Tunawashukuru waliojitahidi kuhudhuria pia tunawatia moyo wengine kujenga tabia
ya kuhudhuria semina muhimu kama hizi.
5. Kamati ya
Majengo Mtaa itakutana Tegeta kanisani siku ya sabato leo (20/04/2013) saa 11
jioni. Wajumbe wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.
6. Makambi ya mtaa yanaanza 21-27/07/2013; tutoe michango
yetu (50,000/) kwa njia ya bahasha, muda unaisha.
7. Sensa ya
washiriki ili kubainisha washiriki waliopo na wasiokuwepo itafanyika sabato
ijayo 27/04/2013. Washiriki pitieni majina ubaoni, kwa ajili ya kuyatambua na
kutoa taarifa kwa Karani/Kamati ya Baraza ya Sensa.
8. Sabato maalum kuchangia ujenzi wa nyumba ya mchungaji itafanyika tarehe 04/05/2013 kanisani Tegeta. Mnenaji
mkuu anategemewa kuwa Pr. Toto Bwire Kusaga kutoka ETC. Goli letu ni kukusanya
fedha si chini ya Milioni Ishirini (Tshs 20,000,000/=). Tunahimiza kila kanisa
lijiandae vyema kwa tukio hilo muhimu.
9. Sadaka maalum ya kusaidia uanzishwaji wa Runinga
(TV) ya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania, Inaendelea kukusanywa
tunahimizwa kila mtu achangie angalau Sh. 10,000/- goli la kanisa letu ni Sh.
3,300,000/-,bado hatujalifikia. Runinga itazinduliwa Juni, 2013.
10. Kesho (21/04/2013) tutakuwa na baraza la kanisa, wakuu wa idara andaeni mipango na
taarifa za kazi, pia kamati mbalimbali malizieni kazi zenu na kuziwasilisha.
11.
Baraza la Mtaa maalum litakaa
tarehe 28/04/2013 kanisani Tegeta saa 3 asubuhi hadi saa 7 kamili mchana. Kikao
hiki ni kwa ajili ya Mchungaji, Wazee wa Kanisa na Makarani wa Kanisa.
Tafadhali zingatieni.
12. Katika ubao wa matangazo, kuna mapendekezo ya:
o MAPENDEKEZO YA BAJETI YA KANISA, 2013
o MAPENDEKEZO YA KALENDA YA MATUKIO YA KANISA, 2013
13. Konferensi yetu – ETC imetenga sabato ya tarehe
20/04/2013 kuwa Siku Kuu ya promosheni ya
kununua na kusambaza kitabu cha “Tumaini Kuu” awamu ya pili. Kila kanisa
linahimizwa kufanya hivyo. Lengo ni kununua vitabu 610,000 na zaidi katika
awamu hii.
14. Juma hili, kuanzai kesho, tutakuwa na juma la uamsho na
Roho ya Unabii, tuhudhurie kila siku saa 11:00, masomo maalumu yamewasili, juma
hili litaendeshwa na Mzee Eraga Mjuli.
15. Maombi ya Jumatano asubuhi yanaendelea saa 11:00
asubuhi, na jioni tunawaalika wote kushiriki.
16. Ndoa: (Mara ya Tatu)
-
Mussa Wilson Sango (Tegeta SDA) na
Agape Denis Bhoke (Kijenge SDA-Arusha), itafungwa 05/05/2013, Mwenge SDA Church.
-
Edger Emir Kapallah (Tegeta SDA) na
Judith George Mabula (Mwanza), itafungwa 27/04/2013, Tegeta SDA Church.
-
Julius Jackson Nywage (Tegeta SDA)
na Dina George Haule (Luhanga SDA-Iringa), itafungwa, 28/04/2013, Mwenge SDA
Church.
17. Zamu:
-
mzee wa zamu: Eraga Mjuli
-
shemasi mkuu wa zamu: Rafiki Msuya
-
Mashemasi wa Zamu (Someni Ubaoni
zamu zenu)
18.
Utaratibu wa Sabato ya leo—Tarehe 20.04.2013

TUKIO
|
TEGETA
|
WATOTO
|
Mhubiri
|
MZEE S.I.M.KAPAYA
|
MAMA MAINGU
|
Mwenyekiti
|
MZEE DAMBA OMARA
|
|
Fungu Kuu na
Ombi
|
MZEE ERAGA MJULI
|
|
Sadaka &
zaka
|
MZEE R.BARIKESHA
|
|
Kufunga Sabato
|
MAMA RAHABU MORRO
|
19.
Utaratibu wa Sabato ijayo—Tarehe 27.04.2013
TUKIO
|
TEGETA
|
WATOTO
|
Mhubiri
|
MZEE ERAGA MJULI
|
MAMA NYAIBAGO
|
Mwenyekiti
|
MWINJ. DICKSON JOSEPH
MIPAWA
|
|
Ombi na Fungu Kuu
|
NDG. ALEX MAFURU
|
|
Sadaka/Zaka
|
NDG. ISAYA CHARLES
|
|
Maombi J5 (Asb.+Jioni)
|
MZEE S.I.M.KAPAYA
|
|
Kufungua Sabato
|
NDG. ELIYA KENANI
|
Post a Comment