TEGETA SDA

TEGETA SDA

KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO –TEGETA TAARIFA YA UTENDAJI WA KAZI ROBO YA KWANZA [JANUARI –MACHI]

Utangulizi:
Tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kwa Roho wake mtakatifu katika kazi yake, “Nayaweza mambo yote katika Yeye anitiaye Nguvu”[Wafilipi 4:13], tumeuone mkono wa Bwana ukitenda kazi kupitia kanisa lake na jinsi alivyookoa watu wake kwa mkono ulionyoshwa.

Idara ya Huduma:
Tumekuwa na efoti ya wiki mbili, [02—16/03/2013], katika viwanja vya kanisa la waadventista wasabato Tegeta. Wahubiri walikuwa ni Mchungaji Dominic Mapima akishirikiana na wana-AMR (Adventist Muslim Relations).
Katika efoti hii masomo yaliyotolewa ni ya;
·      Kaya na familia [Mwinjilisti Modest Mkufu]
·      Tarumbeta za Vitabu [Mwinjilist Straton Chami]
·      Mahubiri ya Neno kuu [Mchungaji Dominic Mapima]
·      Pia tulihudumiwa na wainjilisti: Bertha Lazima, Daniel Ramadhani na Baraka Ndola.
Mahudhurio:
Washiriki
Wageni
Jumla
3.3.13
60
7
67
4.3.13
83
22
105
5.3.13
72
35
107
6.3.13
10
15
25
7.3.13
66
38
104
8.3.13
57
41
98
9.3.13
145
44
189
10.3.13
61
30
91
11.3.13
70
18
88
12.3.13
70
26
96
13.3.13
59
21
80
14.3.13
57
28
85
15.3.13
52
32
84
16.3.13
109
20
129
JUMLA
971
377
1348
WASTANI
69
27
96
S.D. [Mtawanyiko]
30.2
10.5
35.6
Mahudhurio yamekuwa yakibadilikabadilika sana kama yanavyoonekana na kuwa na takwimu ya utawanyiko ya hali ya juu.
Utembeleaji na Ualikaji:
Huduma/Matendo Yaliyofanyika
Idadi
Nyumba zilizotembelewa
177
Watu waliotembelewa
545
Mafundisho yaliyofanyika (majumbani)
22
Vijizuu vilivyotolewa
103
Vitabu vilivyotolewa
22
Maombezi maalumu
19
Madarasa yaliyofunguliwa
10
Jumla ya watu katika madarasa
12
Maeneo Madarasa yalipo:
·      Bahari beach 1
·      Tegeta shule 4
·      Kondo 2
·      Majita Street 3
Kujitoa na Ubatizo:
Jumla ya watu 22 walijitoa kwa ajili ya ubatizo, waliobatizwa ni watu 15.
Michango ya Efoti:
Efoti hii iligharimu, Kiasi cha TAS 5,500,000/, ikiwa ni gharama mbalimbali kwa ajili ya efoti.
Mungu Awabariki!!
Mzee: Saganga M. Kapaya



No comments

Powered by Blogger.