TEGETA SDA

TEGETA SDA

MAWAKILI WA KRISTO


Mwinjilisti: Saganga I.M.Kapaya,
Kutoka
Kanisa la Waadventista Wasabato-Tegeta
Uwakili kwa KRISTO
1 Kor. 4:1-2
Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inapohitajika katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.
Uwakili kwa KRISTO
1 Kor. 9:17, 18
Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili. Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa injili bila gharama,bila kutumia kwa utimilifu uweza wangu nilio nao katika injili
Uwakili kwa KRISTO
1 Pet. 4:10,11
Kila mmoja kwa kadri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema kwa neema mbalimbali za Mungu….ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa YesuKristo….
Uwakili kwa KRISTO
Tit. 1:7,8,9
Maana imempasa askofu(mwangalizi) awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipenda nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu; bali awe mkaribishaji, mpenda wema,mwenye kiasi,mwenye haki, mtakatifu,mwenye kudhibiti nafsi yake, akilishika lile neno la imani vilevile kama alivyofundishwa,apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.
Uwakili kwa KRISTO
Luka 12:42,43
Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote,awape watu posho kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo.
Uwakili kwa KRISTO
Luka 16:1-2
Tena, aliwaambia wanafunzi wake, palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyekuwa na wakili wake; huyu alishitakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake. Akamwita, akamwambia, ni habari gani hii ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya uwakili wako, kwa kuwa huwezi kuwa wakili tena. (inaendelea)
Uwakili kwa KRISTO
Luka 16:9,10
Nami nawaambia, jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele. Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.
Uwakili kwa KRISTO
Spiritual Gifts, Vol.1, p181-182
“Shetani alitumia tamaa, kujipenda nafsi kwa Yuda na kumuongoza kulalamika juu ya marham Mariamu aliyoitoa wakfu kwa Yesu. Yuda aliiangalia kama ufujaji mkubwa; ingeweza kuuzwa na kuwapa maskini. Hakuwajali maskini lakini akahesabu sadaka ile ya ukarimu kwa Yesu kuwa ubadhilifu. (inaendelea)
Uwakili kwa KRISTO
Yuda alimpigia bei Bwana wake kiasi cha kumuuza kwa vipande kidogo vya fedha. Na niliona kuna wengine walio kama Yuda kati ya wale wanaotangaza kumsubiri Bwana wao. Shetani amewashikilkia lakini hawajui. Mungu hawezi kukubali hata chembe kidogo ya tamaa na ubinafsi. Mungu anavichukia na anadharau maombi na kusihi kwa wenye tabia hizo.
Uwakili kwa KRISTO
Ambavyo Shetani anaona muda wake ni mfupi, anawaongoza kuwa wachoyo zaidi na zaidi, wenye tamaa zaidi na baadae anafurahia sana anapowaona wakijikumbatia wenyewe, katika kifungo , ufukara na choyo”.
Uwakili kwa KRISTO
Spiritual Gifts, vol. 1, p182.
“kila aliye mchoyo na mwenye tamaa ataanguka njiani. Yuda aliyemuuza Bwan wake, watauza kanuni bora na kuacha mpango adilifu wa ukarimu kwa mambo kidogo ya kidunia. Wote hao watapepetwa kutoka katika watu wa Mungu. Wale wanaoitaka Mbingu ni lazima, kwa nguvu zote walizo nazo kushikilia kanuni za Mbingu.”
Uwakili kwa KRISTO
Je kama nimekuwa nikimuibia Bwana zaka, nitubuje?
Review and Herald, Jan, 20, 1885.
“mahali popote palipokuwa na hali ya kutojali kufanya sehemu yako kurudisha kwa Bwana sehemu yake, utubu kwa majuto ya rohoni na ufanye kurudisha, ili isije laana yake juu yako…
Uwakili kwa KRISTO
wakati umeshafanya kile uwezavyo kwa upande wako, pasipo kuzuia chochote kinachomhusu Muumba wako, unaweza kuuliza akupatie namana ya kutuma ujumbe/ukweli kwa walimwengu.”
Uwakili kwa KRISTO
Je, Nikiomba msamaha tu, kwa zaka nilizo kula, si inatosha tuu?
Messages to Young People, p. 248.
“Maombi hayakusudiwi kufanya badiliko lolote kwa Mungu; bali huleta upatanifu na Mungu. Maombi hayachukui nafasi ya wajibu. Maombi yaliyotolewa wakati wowote mara kwa mara na tena kwa bidii,
Uwakili kwa KRISTO
kamwe hayatakubalika kwa Mungu yachukue nafasi ya zaka. Maombi hayatalipia madeni yetu kwa Mungu.”
Mungu alituasa: Soma (Wal. 6:1-7)
“…[f4]ndipo itakapokuwa amefanya dhambi, na kupata hatia, atarudisha hicho alichokipata…
  [f6] kisha ataleta sadaka yake ya hatia kwa Bwana.”
Uwakili kwa KRISTO
Je twaweza kuwa tunamdanganya Mungu katika ahadi na matoleo? Wal.6:1-7.
Kudanganya kutokana na mapatano(ahadi),kuapa kwa uongo (ahadi) (f2,3)
Njia pekee ni kurudisha/kutimiza mapatano/kiapo/naziri na kutubia dhambi (f4,5,6)
Uwakili kwa KRISTO
Yesu alituasa nini kuhusu kupatanishwa  na kutubu?:
Math. 5:26.
“Amini, nakuambia, hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.”
Uwakili kwa KRISTO
Je Yesu alikubali toba ya wizi ya Zakayo?
Luka 19:8-9
“…[f8]Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimemnyang’anya mtu kwa hila namrudishia mara nne…
  [f9]Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu,…
Uwakili kwa KRISTO
Je Mungu anajali zaka ndogo?
Math. 23:23
…”mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira…hayo imewapasa kuyafanya wala yale mengine msiyaache.”
Uwakili kwa KRISTO
Mambo gani yanasababisha watu kutokutoa zaka na sadaka kwa uaminifu?
Kutoweka vipaumbele sahihi., Harusi, misiba, maisha. (Math 6:33)
Nira za mikopo na madeni, mabenki, SACCOs, upatu, n.k. (Kum.15:6)
Kukosa imani juu ya matoleo na hofu ya maisha (Luka 18:8, Ebr. 11:6)
Uwakili kwa KRISTO
Ubinafsi, ulafi na choyo (mf. Kijana tajiri, Math. 19:16-22)

Uwakili kwa KRISTO

Je laana ya kutokulipa zaka na sadaka ni ipi?
(Soma Mal. 3:9) na Kumb.28:15-68
Laana juu ya mafanikio (f16-17)
Laana juu ya uzao wako (f18)
Laana ya mashaka na kukemewa (f20)
Laana ya magonjwa; tauni,kifua kikuu, homa, kuwashwa, upanga, ukaufu, koga n.k (f21,22,27,28,35)

Uwakili kwa KRISTO

Laana ya kuibiwa mke/mume,mali (f30)
Laana ya kiuchumi, utakopeshwa (f44)
Laana ya mapigano katika familia na kulana(f54-57)
Laana ya kuzimia, wasiwasi na kudhoofika, woga (f65-68)

Uwakili kwa KRISTO

Je baraka za kulipa zaka na sadaka ni zipi?
Mibaraka ya kufunguliwa madirisha ya Mbinguni (Mal.3:10)
Mibaraka ya chakula, afya, kutokuharibu mimba, ugumba, kuhofiwa, uchumi bora,(Kut. 23:25-27, Kum.28:4-14)
Mibaraka ya utawala/mamlaka (Math.25:21)
Mibaraka ya taji ya uzima wa milele (Uf.2:10)
Uwakili kwa KRISTO
Review and Herald Dec. 1, 1896
“Haitachukua muda mrefu kabla mlango wa rehema kufungwa. Ikiwa hatufanyi sasa jitihada za kumtumikia Bwana kwa uaminifu, jinsi gani utakutana na kumbukumbu yako ya kutotenda kwa uaminifu? Si muda mrefu kuanzia sasa, wito utatolewa kwa ajili ya kusawazisha vitabu vya hesabu na utahitajika kusema,
Uwakili kwa KRISTO
‘kiasi gani unawiwa na Bwana Mungu? Ikiwa hili haliwezi kufanyika, kwa unyenyekevu wenye majuto mwombe Mungu kwa ajili ya Kristo akusamehe deni lako kubwa. Anza sasa kutenda kama mkristo. Usitoe udhuru kwa ajili ya kushindwa kutoa kwa Bwana iliyo sehemu yake. Sasa, wakati bado sauti tamu ya rehema inaposikika, ni wakati bado hujachelewa, kwa makosa uwezayyo kuyasahihisha
Uwakili kwa KRISTO
‘wakati iitwapo leo, kama utaisikia sauti yake; usifanye moyo wako mgumu.”
Selected Messages, Vol. 4, p1893
“Kwa kadri walivyopokea nuru, wengi wamefanya maungamo kuhusiana na madeni wanayowiwa na Mungu, na kuelekeza dhamira zao za kuyaondoa.
Uwakili kwa KRISTO
‘Ibrahimu kwa kutambua deni lake kwa Mungu, anafanya matengenezo na uamuzi thabiti.
Ebr. 7:2“ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote,”
Njia bora ya kutengeneza, ni kupiga thamani ya vitu vyako na kutoa asilimia 10 zaka, 10 sadaka,
 Mapato=Mali+Matumizi.
Uwakili kwa KRISTO
Selected Messages, Vol. 4, p1893
‘Nashauri ya kwamba waweke kwa mhazini ukumbusho wa ahadi zao kulipa kiasi cha zaka ya uaminifu mapema, kadri wawezavyo kupata fedha wafanye hivyo. Vichwa vingi vinapo inamishwa kukubali; mimi nina uhakika mwaka ujao hautakuwa na hazina iliyo tupu kama ilivyo sasa hivi.”
Uwakili kwa KRISTO
WITO:
AMUA LEO KUWA WAKILI MWAMINIFU KWA AJILI YA UZIMA WA MILELE.
MUNGU AKUBARIKI UNAPOFANYA MAAMUZI HAYA YA UMILELE.




No comments

Powered by Blogger.