KARIBUNI KWENYE BLOGU YA KANISA LA TEGETA
Nawasalimu katika jina
la Bwana wetu Yesu Kristo, Karibuni katika blogu ya Kanisa la waadventista
wasabato Tegeta, wakati unaenda mbio, maendeleo pia yanatokea kwa kasi, na sisi
kama wasio wa ulimwengu huu lakini tukiwa ulimwenguni, twasafiri humu, hivyo
tusimame imara katika imani.
Pia tunamshukuru Mungu
kwa ushindi mkuu katika juma la uamsho la uwakili, ambapo mtu 1
aliokolewa na pia katika majuma mawili ya effort ambako watu 15 waliokolewa na
kubatizwa katika maji mengi, kama lilivyo agizo lake Mungu. Mathayo 3:16.
Maendeleo katika
technologia ya mawasiliano na habari yamekuwa ni chachu kubwa kwa Injili ya
Yesu Kristo, nasi kama chombo cha Mungu Duniani, tumepewa ujumbe kuufikisha kwa
watu wote kwa wakati, hivyo teknohama ni jukwaa ambalo twaweza kulitumia kwa
kufanikisha utume wetu. (Math. 28:18-20).
- tegetasdachurch@blogspot.com
- twitter.com/tegetasdachurch
- facebook.com/tegeta.sdachurch
- tegeta.sdachurch@facebook.com
- tegetasdachurch@gmail.com
Wenu Shambani mwa
BWANA, na Mtumwa wake Kristo,
Mwinjilisti: Saganga
M. KAPAYA
Mzee wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Tegeta (2013)
Blog hii inatumika mpaka sasa?by masasi 2017 march 18
ReplyDelete