TEGETA SDA

TEGETA SDA

MATANGAZO YA KANISA, SABATO YA 27/04/2013



1. Tunamshukuru sana Mungu kwa kutulinda kwa wiki nzima hadi Sabato ya leo. Tunawakaribisha wageni kwa wenyeji katika Ibada ya leo.

2.  . Mahubiri  katika Miji Mikuu yanamalizika leo Dodoma. Tunashukuru kwa michango yenu, goli letu lilikuwa 330,000/, tumelipa 200,000/, bado 130,000/ tuchangie na tumalizie ahadi zetu.

3 Kamati ya Majengo Mtaa itakutana Tegeta kanisani siku ya sabato leo (27/04/2013) saa 11 jioni. Wajumbe wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.

4. Makambi ya mtaa yanaanza 21-27/07/2013; tutoe michango yetu (50,000/) kwa njia ya bahasha, muda unaisha., na kupitia viko vyetu vya S.S, waalimu sisitizeni hilo.

5. Sensa ya washiriki ili kubainisha washiriki waliopo na wasiokuwepo itafanyika leo, hivyo tutakuwa na mashauri ya dharura kwa ajili ya kazi hiyo.

6. Sabato maalum kuchangia ujenzi wa nyumba ya mchungaji itafanyika, Sabato ijayo, 04/05/2013 kanisani Tegeta. Mnenaji mkuu anategemewa kuwa Pr. Toto Bwire Kusaga kutoka ETC. Goli letu ni kukusanya fedha si chini ya Milioni Ishirini (Tshs 20,000,000/=). Zingatieni maelekezo yaliyotolewa na Mzee Damba.

7. Sadaka maalum ya kusaidia uanzishwaji wa Runinga (TV) ya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania, Inaendelea kukusanywa tunahimizwa kila mtu achangie angalau Sh. 10,000/- goli la kanisa letu ni Sh. 3,300,000/-,bado hatujalifikia. Runinga itazinduliwa Juni, 2013.

8. Leo, saa 8:30—9:30, tutakuwa na baraza la kanisa, la dharura, wakuu wa idara andaeni mipango na taarifa za kazi, pia kamati mbalimbali malizieni kazi zenu na kuziwasilisha.

9. Baraza la Mtaa maalum litakaa kesho, (28/04/2013) kanisani Tegeta saa 3 asubuhi hadi saa 7 kamili mchana. Kikao hiki ni kwa ajili ya Mchungaji, Wazee wa Kanisa na Makarani wa Kanisa. Tafadhali zingatieni.

10. Leo, tunahitimisha, juma la uamsho na Roho ya Unabii, juma hili liliendeshwa na Mzee Eraga Mjuli, hivyo leo tunaanza kuchangia ununuzi wa vitabu vya “Tumaini Kuu” Lengo ni kununua vitabu 610,000 na zaidi katika awamu hii.

11. Maombi ya Jumatano asubuhi yanaendelea saa 11:00 asubuhi, na jioni tunawaalika wote kushiriki.

12. Kupitisha majina ya wanakwaya, walioomba kuimba 2013. (karani)

13. Katika ubao wa matangazo, kuna mapendekezo ya:

o    MAPENDEKEZO YA BAJETI YA KANISA, 2013
o    MAPENDEKEZO YA KALENDA YA MATUKIO YA KANISA, 2013

14. Kwaya yetu ya kanisa, kesho jumapili, itaenda Bagamoyo, kushiriki mwaliko, katika ibada ya kuzindua kanda ya kanisa la Bagamoyo, mzee msuya atakuwa ndiye kiongozi wa msafara.

15. Ndoa: Mwaliko katika Ibada ya Ndoa.
-          Edger Emir Kapallah (Tegeta SDA) na Judith George Mabula (Mwanza), itafungwa leo, saa 10:00, jioni, Tegeta SDA Church, munakaribishwa, ndoa itafungwa na Mch. Robinson Nkoko.
-          Julius Jackson Nywage (Tegeta SDA) na Dina George Haule (Luhanga SDA-Iringa), iliyokuwa ifungwe, 28/04/2013, Mwenge SDA Church., imeahirishwa mpaka mtakapo taarifiwa tena.

16. Uhamisho: (Mara ya 1)
-          Fridson Mkama (554) toka Tegeta kwenda Salasala, DSM
-          Anastanzia Mkama (70) toka Tegeta kwenda Salasala, DSM
-          Paschal Mabula (984) toka Tegeta kwenda Makoko, Musoma

17. Tanzia: Mchungaji J.R.Nyaibago amefiwa na shemeji yake, amesafiri Musoma kwa
       maziko, tuikumbuke familia yake katika maombi

17. Zamu:
-          mzee wa zamu: Saganga I.M. Kapaya
-          shemasi mkuu wa zamu: Eliya Kenani
-          Mashemasi wa Zamu (Someni Ubaoni zamu zenu)

18. Utaratibu wa Sabato ya leo—Tarehe 27.04.2013
TUKIO
TEGETA
WATOTO
Mhubiri
MZEE ERAGA MJULI
MAMA NYAIBAGO
Mwenyekiti
MWINJ. DICKSON JOSEPH MIPAWA

Fungu Kuu na Ombi
MZEE RICHARCH BARIKESHA

Sadaka & zaka
NDG. ISAYA CHARLES

Kufunga Sabato
NDG. ANANIA MASASI


19. Utaratibu wa Sabato ijayo—Tarehe 04.05.2013
TUKIO
TEGETA
WATOTO
Mhubiri
MCHUNGAJI TOTO KUSAGA (ETC)
JOSEPH KALEB
Mwenyekiti
SABATO/MTAA

Ombi na Fungu Kuu
SABATO/MTAA

Sadaka/Zaka
SABATO/MTAA

Maombi J5 (Jioni)
MZEE S.I.M.KAPAYA

Maombi J5 (Asubuhi)
MZEE DAMBA OMARA

Kufungua Sabato
NDG. B.I.MORRO

No comments

Powered by Blogger.