MATANGAZO YA KANISA YA SABATO YA TAREHE 31/08/2013
MATANGAZO YA KANISA: 31/08/2013
1.
Tunamshukuru na kumtukuza Mungu wetu kwa neema na mibaraka
yake, Wageni kwa wenyeji karibuni katika kanisa la Mungu na Ibada takatifu.
2.
(KUPITISHA
WANATENDAKAZI) Tunapenda kuwapongeza wale waliokubali kumtumikia Mungu kwa
nyadhifa mbalimbali kanisani.
3.
Effort yetu ya mtaa itaanza 5-19/10/013.Tafadhali
tuendelea kutoa michango yetu ili kukamilisha na kufanikisha effort hiyo.
Tutachangia 4,000,000/
4.
(TAARIFA: KIWANJA CHA
KONDO), kiwanja chetu cha Kondo, kimevamiwa na Kanisa la Walokole. tunaendelea
kufuatilia hati za kiwanja wizarani ili kupewa umiliki kamili. Tuliombee jambo
hili kwa bidii. 1,200,000/=
5.
Tarehe 8/9/2013. Mtaa wetu wa Tegeta, tutakuwa na ugeni
maalumu kutoka, G.C. (Mashauri kuu ya Kanisa), Makamu mwenza wa mwenyekiti wa G.C. Mch.
Geofrey Mbwana, atakuja kuweka jiwe la msingi la Nyumba la Mchungaji. Kanisa
letu tunahitaji kuchangia 770,000/= kuchangia tukio hilo.
6.
Marekebisho ya choo, hali yake siyo nzuri, tunahitaji
kuchangia 250,000/= kwa ajili ya marekebisho ya choo. Kuweka masinki ya
kuflashi na mabomba.
Ø Jumla ya fedha
yote inayohitajika wiki hii ni; 1,200,000+770,000+250,000=2,220,000/
7.
Tuandae taarifa zote za robo ya 3 na ziletwe kwa mchungaji mwisho Tarehe 15/09/13.
Robo hii ya tatu
8.
Tutakuwa na baraza la kanisa, la dharura kesho saa 1:00 asubuhi.
Tuhudhurie kwa wakati.
9.
Kutakuwa na kambi la Vijana (Masterguide Convention),
Kampala, Bugema University. 4-8/12/20013.
a.
Gharama ni kiingilio $7 (kama TAS 11,327), malazi/chakula $7.5
(kama TAS 12,136) kwa siku, au malazi peke yake $3 (kama TAS 4,854), pia usafiri mpaka kampala makanisa yatajitegemea. Kama
utashiriki matukio yote mawili kiingilio ni $12 badala ya $14. Kanisa
tushirikiane kuwawezesha vijana
10.
Kutakuwa na kongamano la muziki, Kampala, Bugema University.
9-15/12/20013,
a.
Gharama ni kiingilio $7 (kama TAS 11,327) kwa siku, au malazi
peke yake $3 (kama TAS 4,854), pia
usafiri mpaka kampala makanisa yatajitegemea. Kama utashiriki matukio
yote mawili kiingilio ni $12 badala ya $14.,
b.
Ndg. Isaac Webi ameteuliwa kuratibu mpango huo kwa kanisa letu.
Muoneni kwa maelezo zaidi. waimbaji na viongozi wa muziki kanisani, jiandaeni
kwa kuhudhuria, Kanisa tushirikiane kuwawezesha wanamuziki wa kanisa.
c.
Kwa maelezo zaidi kuhusu matukio haya tembeleeni, wavuti ya
divisheni: http://www.ecd.adventist.org
11.
Tarehe leo ni sabato ya idara ya wana wa kike: msisitizo wa
kuzuia unyanyasaji, SASABASI! (END IT NOW!). Mchana tutakuwa na somo hilo
maalumu, na pia taarifa ya waliokwenda Kigali. Karibuni nyote
12. Wagonjwa:
a. Mama Daktari Andrew, anaumwa, yuko nyumbani,
b. Bi Upendo Maingu anaumwa, yuko nyumani,
c.
Mzee Joseph Msuya
anaumwa,
Ø
tuwatembelee na kumuombea ili kuwafariji
13. Matoleo: ya sabato iliyopita ni:…………………………………….
14. Zamu: Mzee wa zamu; Mzee
Damba Omara. Shemasi Mkuu wa zamu, Mzee Elia Kenani.
15. Ratiba Fupi ya Wahudumu:

HUDUMA HUSIKA
|
MHUDUMU (SABATO
LEO, 24/08/2013)
|
MHUDUMU (SABATO
IJAYO, 31/08/2013)
|
Mhubiri
(Watoto)
|
Ndg. Isaya Charles
|
Bi. Rafiki Msuya
|
Mhubiri
(Wakubwa)
|
Mch. John R.Nyaibago
|
Mzee Damba Omara
|
Mwenyekiti
|
Ndg. Anania Mndeme
|
Mzee Elia Kenani
|
Fungu Kuu na
Ombi
|
Ndg. Enock Nyange
|
Ndg. Anania Mndeme
|
Sadaka &
zaka
|
Ndg. Amos Obadia
|
Ndg. Isaya Charles
|
Kufunga Sabato
|
Ndg. Anania Mndeme
|
|
Jumatano (Asb)
|
Mzee Damba Omara
|
|
Jumatano
(Jioni)
|
Ndg. Anania Masasi
|
|
Kufungua Sabato
|
Mwj. Editha Sanga
|
|
Ahsanteni, Mungu
Awabariki!
MAELEKEZO YA MCHUNGAJI TANGAZO NA 5:
SEPT 8,2013 Itakuwa siku maalum katika mtaa
wetu wa Tegeta.Ni siku ya kuweka jiwe la
msingi na kuleta michango yetu ya kumalizia ujenzi wa Nyumba ya mchungaji.Siku
hiyo itaongozwa na Kiongozi wetu wa kanisa katika ngazi ya Ulimwengu mch.Geofrey
Mbwana ambaye ni makamu wa Mwenyekiti wa GC.
Pamoja naye watakuwepo wageni toka Tanzania
Union na Toka Conf.yetu ya ETC.Wageni wengine tunaowategemea ni wachungaji na
Wazee au wakilishi toka
katika mitaa ya Dar.
Pia Kwaya ya Mbiu pamoja na Pf toka kanisa
la Kimanga watakaoendesha Gwaride maalum la kukaribisha wageni. Kutakuwepo pia
wageni mbalimbali walioalikwa kwa ajili ya siku hiyo.
Kwa sababu ya umuhimu wa siku hiyo, Tunawaomba
vijana wetu wakiongozwa na kamanda wetu wa mtaa ndg Nehemia Ibrahamu kuandaa progrm maalum
ya kukaribisha wageni; Kwaya zetu zote za makanisa toka mtaani wajiendee
kushirikiana na kwaya ngeni katika programu maaalum ya uimbaji chini ya kiongozi wa kwaya mtaa
ndg Isaac Webi katika siku hiyo Itapendeza mkiwa katika unifomu.
Program zetu zitaanza saa 2.00- saa 8.00
mchana. Tunatiwa moyo kubeba kipoza njaa ili kufanya utulivu katika siku hiyo. Hebu
tutiane moyo washiriki wote wa mtaa wa Tegeta wadogo kwa wakubwa kuhudhuria
Sherehe hii kubwa ya Kiroho.
Hii imekuja kuimarisha umoja wetu pia. Kumbuka
ni kile ambacho kwa neema ya Bwana tumekifanya cha Kuasisi ujenzi wa Nyumba ya mch.na tumekuwa wa kwanza kuitikia jambo hili
la muhimu katika Conf. Yetu na wameamua kualika mitaa mingine kuja kujifunza
kwetu. Hebu sasa tuje kwa kishindo kumalizia kazi hii. Ukiweza kuaalika hata
marafiki wasio Waadventista njoo nao itakuwa ni ibada ya pekee siku hiyo.
Kamati mbali mbali za maandalizi ya tukio hili kubwa tafadhali tuwajibike
kama tulivyokubaliana katika baraza la mtaa ili kufanikisha maandalizi.Tunatiwa
moyo ili kutoa michango yetu kidogo ili kukaribisha wageni wa siku hiyo.Kumbuka
dalili moja ya mji ulio na baraka ni kutembelewa na wageni.N a neno la Mungu
linatukumbusha kuwa “Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine
wamewakaribisha malaika pasipo kujua.” Webr 13:2
Post a Comment