MATANGAZO YA KANISA YA SABATO YA TAREHE 24/08/2013
MATANGAZO YA KANISA: 24/08/2013
1.
Tunamshukuru na kumtukuza Mungu wetu kwa neema na mibaraka
yake, tunamshukuru kwa kutupa makambi mwaka huu. Wageni kwa wenyeji karibuni
katika kanisa la Mungu na Ibada takatifu.
2.
(KUWAPOKEA WABATIZWA) Tunamtukuza Mungu kwa kanisa kupata
washiriki wapya waliompokea Yesu na kubatizwa (idad 3)
3.
(KUPITISHA WANAKWAYA) Tunapenda kuwapongeza wale walioamua
kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Tunawakaribisha wengine pia.
4.
(TAARIFA: KIWANJA CHA KONDO), kiwanja chetu cha Kondo,
kimevamiwa na Kanisa la Walokole. tunaendelea kufuatilia hati za kiwanja
wizarani ili kupewa umiliki kamili. Tuliombee jambo hili kwa bidii.
5.
Effort yetu ya mtaa itaanza 5-19/10/013.Tafadhali
tuendelea kutoa michango yetu ili kukamilisha na kufanikisha effort hiyo. Goli
la kanisa letu ni 4,000,000/
6.
Tuandae taarifa zote za robo ya 3 na ziletwe kwa mchungaji mwisho Tarehe 15/09/13.
Robo hii ya tatu
7.
Kamati za makambi, yaliyomalizika andaeni taarifa kwa
ajili kuzileta katika katika kikao cha mtaa. Kikao cha mtaa cha kawaida kwa
robo kitafanyika, kesho 24/08/2013
katika kanisa la Tegeta.
8.
Leo, mchana saa 8:00, tutakuwa na washa (semina), ya neno la
Mungu, Unabii. Tujiandae kwa ajili ya kujifunza, wabatizwa wapya muhudhurie
bila kukosa.
9.
Tutakuwa na baraza la kanisa, la dharura leo jioni, saa 10:00
Tuhudhurie kwa wakati.
10.
Kutakuwa na kambi la Vijana (Masterguide Convention),
Kampala, Bugema University. 4-8/12/20013.
a.
Gharama ni kiingilio $7 (kama TAS 11,327), malazi/chakula $7.5
(kama TAS 12,136) kwa siku, au malazi peke yake $3 (kama TAS 4,854), pia usafiri mpaka kampala makanisa yatajitegemea. Kama
utashiriki matukio yote mawili kiingilio ni $12 badala ya $14. Kanisa
tushirikiane kuwawezesha vijana
11.
Kutakuwa na kongamano la muziki, Kampala, Bugema University.
9-15/12/20013,
a.
Gharama ni kiingilio $7 (kama TAS 11,327) kwa siku, au malazi
peke yake $3 (kama TAS 4,854), pia
usafiri mpaka kampala makanisa yatajitegemea. Kama utashiriki matukio
yote mawili kiingilio ni $12 badala ya $14.,
b.
Ndg. Isaac Webi ameteuliwa kuratibu mpango huo kwa kanisa letu.
Muoneni kwa maelezo zaidi. waimbaji na viongozi wa muziki kanisani, jiandaeni
kwa kuhudhuria, Kanisa tushirikiane kuwawezesha wanamuziki wa kanisa.
c.
Kwa maelezo zaidi kuhusu matukio haya tembeleeni, wavuti ya
divisheni: http://www.ecd.adventist.org
12.
Tarehe 3/9/2013 ni sabato ya idara ya wana wa kike: msisitizo
wa kuzuia unyanyasaji, SASABASI! (END IT NOW!). Somo limewasili, idara ya wana
wa kike tunawaomba mjiandae, sabato ijayo tutakuwa na somo hilo maalumu.
13.
Wagonjwa: Mama Daktari
Andrew, amefanyiwa upasuaji, hospitali ya Lugalo, tumuombee na kumtembelea ili kumfariji.
Bi Joyce /Malima
Martin, anaumwa, washiriki tunombwa tumtembelee kwake, Nyaishozi (chasimba?) na
kumfariji.
14. Matoleo: ya sabato iliyopita ni:…………………………………….
15. Zamu: Mzee wa zamu; Mzee
Saganga Kapaya. Shemasi Mkuu wa zamu, Mzee
Elia Kenani.
16. Ratiba Fupi ya Wahudumu:
HUDUMA HUSIKA
|
MHUDUMU (SABATO
LEO, 24/08/2013)
|
MHUDUMU (SABATO
IJAYO, 31/08/2013)
|
Mhubiri
(Watoto)
|
Bi. Upendo Maingu
|
Mzee Joseph Msuya
|
Mhubiri
(Wakubwa)
|
Ndg. Daudi Kubhoja
|
Ndg. Fred Maiga
|
Mwenyekiti
|
Mzee B.I.Morro
|
Ndg. Anania Mndeme
|
Fungu Kuu na
Ombi
|
Mzee Damba Omara
|
Ndg. Enock Nyange
|
Sadaka &
zaka
|
Ndg. Anania Masasi
|
Ndg. Amos Obadia
|
Kufunga Sabato
|
Mzee John Kamuli
|
Ndg. Anania Mndeme
|
Jumatano (Asb)
|
Mzee Zihirwani
Chikira
|
|
Jumatano
(Jioni)
|
Ndg. Anania Masasi
|
|
Kufungua Sabato
|
Ndg. Daudi Kubhoja
|
|
Ahsanteni, Mungu
Awabariki!
Post a Comment