TEGETA SDA

TEGETA SDA

MATANGAZO YA KANISA YA SABATO YA 11/05/2013



1. Tunamshukuru sana Mungu kwa kutulinda kwa wiki nzima hadi Sabato ya leo. Tunawakaribisha wageni kwa wenyeji katika Ibada ya leo.

2. Makambi ya mtaa yanaanza 21-27/07/2013; tutoe michango yetu (50,000/) kwa njia ya bahasha, muda unaisha., na kupitia vikosi vyetu vya S.S, waalimu sisitizeni hilo.

3 Tunawashukuru washiriki kwa kutoa ahadi zenu kwa Mungu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mchungaji. Tunawasihi muendelee kutimiza ahadi zenu kama mlivyoahidi, ili ujenzi uendelee. Tumia bahasha kuwasilisha michango hiyo kwa kuanduka majengo mtaa, au onana na mhazini kutoa mchango wako.

4.Jumapili iliyopita, tulikuwa na semina ya Uwakili, semina iliendeshwa na mch.T.Kusaga toka ETC.,  Leo, saa 8:30 mchana, Mzee Fundi Makama na Mama Egla Mgeta, watatuletea semina hiyo tena; karibuni ni Muhimu sana.

5. Sadaka maalum ya kusaidia uanzishwaji wa Runinga (TV) ya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania, Inaendelea kukusanywa tunahimizwa kila mtu achangie angalau Sh. 10,000/- goli la kanisa letu ni Sh. 3,300,000/-,bado hatujalifikia. Runinga itazinduliwa Juni, 2013.

6. Sensa ya washiriki inaendelea katika Tanzania Union.kila mshiriki hakikisha kuwa kama ushirika wako haupo katika kanisa unalosali,wasiliana na karani wa kanisa ili kuagiza ushirika wako,vinginevyo baada ya miezi 3,washiriki wasiojulikana wataondolewa katika vitabu vya Ushirika

7. Tunawakumbusha washiriki kuendelea kutimiza ahasi zenu kwa kuchangia ununuzi wa vitabu vya “Tumaini Kuu” Lengo ni kununua vitabu 610,000 na zaidi katika awamu hii. Kila kitabu ni 2000/ tu

8. Kongresi ya wasichana, umri wa miaka 15 na kuendelea, itafanyika Morogoro, Kitungwa Sekondari, tarehe 18-22/06/2013; Gharama ni kiingilio 5,000/, malazi 5,000/ na nauli ya kwenda Morogoro na kurudi, Chakula Konferensi itagharimikia; wasichana wote wanahamasishwa kuhudhuria, onaneni na uongozi wa kanisa kwa maelekezo zaidi.

9. Maombi ya Jumatano asubuhi yanaendelea saa 11:00 asubuhi, na jioni tunawaalika wote kushiriki

10. Kupitisha majina ya wanakwaya, walioomba kuimba 2013. (karani Anania Masasi)

11. Sabato ijayo ya 18/05/2013, tutakuwa na chagizo kwa ajili ya maandalizi ya efoti ya idara ya Afya na Kiasi, itakayofanyika May 25 mpaka Juni 1, gharama yake ni 3,735,000/, tunawaomba kuandaa michango yenu. Katika wiki hii mafunzo ya afya, kiasi, mapishi na neno la Mungu yatatolewa, wanenaji wanatarajiwa kuwa ni mwinjilisti Marema (Morogoro) na mama Esperansa Odhiambo na Familia ya Wamishionari (DSM)

12. wanachama wa DORKAS na AMO kanisani, munaombwa na viongozi wenu kubaki mara ya ibada.

13. Zamu:
-          Mzee wa zamu: Mzee Joseph Msuya
-          Shemasi mkuu wa zamu: Mzee Eliya Kenani
-          Mashemasi wa Zamu (Someni Ubaoni zamu zenu)


14. Utaratibu wa Sabato ya leo—Tarehe 11.05.2013


 
TUKIO
TEGETA
WATOTO
Mhubiri
MZEE JOSEPH MSUYA
S.I.M.KAPAYA
Mwenyekiti
NDG. ANANIA MASASI

Fungu Kuu na Ombi
NDG. BAMBINO P. NYAMBITA

Sadaka & zaka
MZEE RICHARD. BARIKESHA

Kufunga Sabato
MWJ  EDGAR  E. KAPALA


15. Utaratibu wa Sabato ijayo—Tarehe 18.05.2013

TUKIO
TEGETA
WATOTO
Mhubiri
MWJ. MOFATI
MAMA RAHABU MORRO
Mwenyekiti
NDG. BAMBINO P.NYAMBITA

Ombi na Fungu Kuu
NDG. E.LIA KENANI

Sadaka/Zaka
NDG. DAUDI KUBOJA

Maombi J5 (Jioni)
MZEE ERAGA MJULI

Maombi J5 (Asubuhi)
MZEE ERAGA MJULI

Kufungua Sabato
NDG. EDGAR E. KAPALA


16. Ratiba Fupi ya Mchungaji ni kama ifuatavyo:
MWEZI
TAREHE
SEHEMU HUSIKA
TUKIO

12
Madala
Baraza la kanisa
Mei
14-18
Mbweni
Uamsho

24-31
Boko
Uamsho  


No comments

Powered by Blogger.