TEGETA SDA

TEGETA SDA

MATANGAZO YA KANISA YA SABATO YA TAREHE 18/05/2013



1. Tunamshukuru sana Mungu kwa kutulinda kwa wiki nzima hadi Sabato ya leo. Tunawakaribisha wageni kwa wenyeji katika Ibada ya leo.

2. Makambi ya mtaa yanaanza 21-27/07/2013; tutoe michango yetu (50,000/) kwa njia ya bahasha, muda unaisha., na kupitia vikosi vyetu vya S.S, waalimu sisitizeni hilo.

3 Tunawashukuru washiriki kwa kutoa ahadi zenu kwa Mungu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mchungaji. Tunawasihi muendelee kutimiza ahadi zenu kama mlivyoahidi, ili ujenzi uendelee. Tumia bahasha kuwasilisha michango hiyo kwa kuanduka majengo mtaa, au onana na mhazini kutoa mchango wako.

4. Sadaka maalum ya kusaidia uanzishwaji wa Runinga (TV) ya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania, Inaendelea kukusanywa tunahimizwa kila mtu achangie angalau Sh. 10,000/- goli la kanisa letu ni Sh. 3,300,000/-,bado hatujalifikia. Runinga itazinduliwa Juni, 2013.

5. Tunawakumbusha washiriki kuendelea kutimiza ahadi zenu kwa kuchangia ununuzi wa vitabu vya “Tumaini Kuu” Lengo ni kununua vitabu 610,000 na zaidi katika awamu hii. Kila kitabu ni 2000/ tu

6. Sensa ya washiriki inaendelea katika Tanzania Union.kila mshiriki hakikisha kuwa kama ushirika wako haupo katika kanisa unalosali,wasiliana na karani wa kanisa ili kuagiza ushirika wako,vinginevyo baada ya miezi 3,washiriki wasiojulikana wataondolewa katika vitabu vya Ushirika

7. Kutakuwa na ubatizo mkuu wa robo ya pili, tarehe 01/06/013. Wale wote ambao mutahitaji ubatizo tunawasihi muonane na wazee wa kanisa, leo mchna kwa ajili ya kupewa maelekezo.

8. Kongresi ya wasichana, umri wa miaka 15 na kuendelea, itafanyika Morogoro, Kitungwa Sekondari, tarehe 18-22/06/2013; Gharama ni kiingilio 5,000/, malazi 5,000/ na nauli ya kwenda Morogoro na kurudi, Chakula Konferensi itagharimikia; wasichana wote wanahamasishwa kuhudhuria, onaneni na uongozi wa kanisa kwa maelekezo zaidi.

9. Tutakuwa na baraza la kanisa la kawaida, kesho, tarehe 19/05/2013, kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 7 mchana, tunawasihi wakuu wa idara muje na taarifa zenu za kazi za mwezi, ni muhimu sana.

10. Tutakuwa na baraza la mtaa 02/06/2013 Litakalokutana Tegeta kanisani muda ni saa 3.00 kamili.Tafadhali tujipange kuhudhuria na taarifa zetu mbali mbali hasa za makambi na uinjilisti.

10. Juma la maombi ya ECD Litaanza Mei 25-June 1.Katika makanisa yote ya. Bado hatujapata masomo ya juma hilo, yakifika tutawajulisheni. Tujiandae kushiriki mibaraka mikubwa iliyo mbele yetu.

11. Kutakuwa na kambi la uwakili katika kanda zote za Dar es Salaam litakalofanyikia Temeke kuanzia 09-16/2013.Wahiriki wa kambi hilo ni Wachungaji,Wazee wa kanisa, Viongozi wa uwakili, Majengo, Wahazini wa makanisa.Tujipange kuhudhuria kambi hilo ni muhimu, litasimamiwa na viongozi wa Divisheni, Unioni na Konferensi

12. Leo ni sabato ya kuchangia effort ya idara ya afya na kiasi inayoanza wiki ijayo jumamosi kwa muda wa juma moja. tunawasihi ndg washiriki tutoe kwa mioyo
yenye ukarimu na kusudio ili tuifanye kazi ya bwana. kwa wale ambao mmekwisha kutoa chochote kwa ajili ya effort hii si vibaya tukajumuika tena kuongezea
maana goal letu bado halijatimia .tunatafuta sh 3,575,000/=.Mungu awabariki.


13. Maombi ya Jumatano na Jumapili asubuhi yanaendelea saa 11:00 asubuhi, na Jumatano jioni saa 11:00; tunawaalika wote kushiriki

14. Zamu:
-          Mzee wa zamu: Mzee S.I.M. Kapaya
-          Shemasi mkuu wa zamu: Mama Rafiki Msuya
-          Mashemasi wa Zamu:[ubaoni]

15. Tanzia:

-- Familia ya mzee wa kanisa Eraga Mjuli, wamefiwa na baba mdogo wa mzee Eraga Mjuli, mzee Eraga kasafiri kwenda Mwanza kwa maziko, tuwaombee na kuwafariji.

-- Familia ya mzee Mauma wamefiwa na mtoto wa ndugu yake mzee Mauma, wamesafirisha kwenda Musoma kwa maziko, tuwaombee na kuwafariji.

16. Utaratibu wa Sabato ya leo—Tarehe 18.05.2013


 
TUKIO
TEGETA
WATOTO
Mhubiri
MWJ. MOFATI
MAMA RAHABU MORRO
Mwenyekiti
MZEE RICHARD BARIKESHA

Fungu Kuu na Ombi
NDG. E.LIA KENANI

Sadaka & zaka
NDG. DAUDI KUBOJA

Kufunga Sabato
NDG. ADAM MSAKU


17. Utaratibu wa Sabato ijayo—Tarehe 25.05.2013

TUKIO
TEGETA
WATOTO
Mhubiri
MWJ MALEMA
MAMA MAINGU JANDWA
Mwenyekiti
MZEE S.I.M. KAPAYA

Ombi na Fungu Kuu
MZEE B.I.MORRO

Sadaka/Zaka
NDG ANANIA MNDEME

Maombi J5 (Jioni)
MZEE JOSEPH MSUYA

Maombi J5 (Asubuhi)
MZEE JOSEPH MSUYA

Kufungua Sabato
NDG. GEOFREY MPEMBENI


18. Ratiba Fupi ya Mchungaji ni kama ifuatavyo:

MWEZI
TAREHE
SEHEMU HUSIKA
TUKIO

12
Madala
Baraza la kanisa
Mei
14-18
Mbweni
Uamsho

24-31
Boko
Uamsho  
Juni
01-08
Tegeta
Uamsho

09-16
Temeke
Kambi la uwakili

18-22
Kisanga
Uamsho

25-30
Bunju
Uamsho

19. Ratiba ya Mabaraza ya Uhai ya Kila Robo-II

KANISA HUSIKA
BARAZA LA KANISA
BARAZA LA MASHAURI YA KANISA
TAREHE
MUDA
TAREHE
MUDA
BOKO
23/6/2013
1.00-7.00
30/06/13
8.00-12.00
BUNJU
30/6/2013
1.00-7.00
07/07/13
1.00-7.00
KISANGA
19/5/2013
1.00-7.00
26/05/13
8.00-12.00
MADALA
09/6/2013
1.00-7.00
17/06/13
8.00-12.00
MBWENI
26/5/2013
1.00-7.00
02/06/13
8.00-12.00
TEGETA
16/6/2013
1.00-7.00
23/06/13
8.00-12.00
BARAZA-MTAA
02/6/2013
3.00-8.00
HAKUNA
HAKUNA


Ahsanteni na Mungu Awabariki!!

No comments

Powered by Blogger.