TEGETA SDA

TEGETA SDA

MATANGAZO YA KANISA YA SABATO YA TAREHE 25/05/2013



1. Tunamshukuru sana Mungu kwa kutulinda kwa wiki nzima hadi Sabato ya leo. Tunawakaribisha wageni kwa wenyeji katika Ibada ya leo.

2. Makambi ya mtaa yanaanza 21-27/07/2013; tutoe michango yetu (50,000/) kwa njia ya bahasha, muda unaisha., na kupitia vikosi vyetu vya S.S, waalimu sisitizeni hilo.

3 Tunawashukuru washiriki kwa kutoa ahadi zenu kwa Mungu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mchungaji. Tunawasihi muendelee kutimiza ahadi zenu kama mlivyoahidi, ili ujenzi uendelee. Tumia bahasha kuwasilisha michango hiyo kwa kuanduka majengo mtaa, au onana na mhazini kutoa mchango wako.

4. Sadaka maalum ya kusaidia uanzishwaji wa Runinga (TV) ya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania, Inaendelea kukusanywa tunahimizwa kila mtu achangie angalau Sh. 10,000/- goli la kanisa letu ni Sh. 3,300,000/-,bado hatujalifikia. Runinga itazinduliwa Juni, 2013.

5. Tunawakumbusha washiriki kuendelea kutimiza ahadi zenu kwa kuchangia ununuzi wa vitabu vya “Tumaini Kuu” Lengo ni kununua vitabu 610,000 na zaidi katika awamu hii. Kila kitabu ni 2000/ tu

6. Sensa ya washiriki inaendelea katika Tanzania Union.kila mshiriki hakikisha kuwa kama ushirika wako haupo katika kanisa unalosali,wasiliana na karani wa kanisa ili kuagiza ushirika wako,vinginevyo baada ya miezi 3,washiriki wasiojulikana wataondolewa katika vitabu vya Ushirika

7. Kutakuwa na ubatizo mkuu wa robo ya pili, tarehe 01/06/013. Saa 9 mchana, Wale wote ambao mutahitaji ubatizo tunawasihi muonane na wazee wa kanisa, leo mchna kwa ajili ya kupewa maelekezo.

8. Kongresi ya wasichana, umri wa miaka 15 na kuendelea, itafanyika Morogoro, Kitungwa Sekondari, tarehe 18-22/06/2013; Gharama ni kiingilio 5,000/, malazi 5,000/ na nauli ya kwenda Morogoro na kurudi, Chakula Konferensi itagharimikia; wasichana wote wanahamasishwa kuhudhuria, onaneni na uongozi wa kanisa kwa maelekezo zaidi.

9. Tutakuwa na baraza la kanisa la dharura, leo, mchana, tarehe 25/05/2013, kuanzia saa 8 mchana, ni muhimu sana, tuhudhurie kwa wakati.

10. Tutakuwa na baraza la mtaa 02/06/2013 Litakalokutana Tegeta kanisani muda ni saa 3.00 kamili.Tafadhali tujipange kuhudhuria na taarifa zetu mbali mbali hasa za makambi na uinjilisti.

10. Juma la maombi ya ECD Litaanza Mei 25-June 1.Katika makanisa yote ya. Bado hatujapata masomo ya juma hilo, yakifika tutawajulisheni. Tujiandae kushiriki mibaraka mikubwa iliyo mbele yetu.

11. Kutakuwa na kambi la uwakili katika kanda zote za Dar es Salaam litakalofanyikia Temeke kuanzia 09-16/6/2013.Wahiriki wa kambi hilo ni Wachungaji,Wazee wa kanisa, Viongozi wa uwakili, Majengo, Wahazini wa makanisa.Tujipange kuhudhuria kambi hilo ni muhimu, litasimamiwa na viongozi wa Divisheni, Unioni na Konferensi

12. Leo ni sabato ya kuchangia effort ya idara ya afya na kiasi inayoanza wiki ijayo jumamosi kwa muda wa juma moja. tunawasihi ndg washiriki tutoe kwa mioyo yenye ukarimu na kusudio ili tuifanye kazi ya bwana. kwa wale ambao mmekwisha kutoa chochote kwa ajili ya effort hii si vibaya tukajumuika tena kuongezea maana goal letu bado halijatimia .tunatafuta sh 3,575,000/=.Mungu awabariki.

13. Kanuni mpya za mwaka 2010 za kiswahili zimeishatoka,Bei ni Tshs.8000.Fanya mpango kupitia idara ya uchapishaji kanisani upate kopi yako.

14. Kuanzia June 02-08,2013 Ni juma maalum la huduma za Idara ya wanawake.Tumia siku za Maombi ya Jumatano, na Ijumaa kwa ajili ya masomo. Kuna somo maallum litakalohitimishwa siku ya Jumamosi ya 8,. Pia sadaka maalum ya kusaidia wanawake kielimu itatolewa.

15. Tunawatangazia wana AMO/Dorcas wote kuwa: Mazoezi ya kwaya ya AMO/Dorkas  yataanza hivi karibuni, tunaomba  wale  wote watakaopenda kujiunga  na  kwaya hii walete majina  yao  kwa kiongozi  wa  Dorkas na  Kiongozi wa AMO. Siku  ya mazoezi  itatangazwa  hapo baadaye.

15. Tunapenda kuwatangazia kwamba katika mbao za matangazo ya kanisa, pia kwenye blog, na pia kupitia mitandao yetu ya jamii, tumeweka mapendekezo ya “Master Plan” ya kanisa letu, tunawaomba muipitie, na kutoa mapendekezo kupitia: uongozi wa kanisa, boksi la maoni, au barua pepe ya kanisa, au mitandao ya jamii.

14. Zamu:
-          Mzee wa zamu: Mzee Damba Omara
-          Shemasi mkuu wa zamu: Mzee Eliya Kenani
-          Mashemasi wa Zamu:[ubaoni]

15. Wagonjwa:

-- Mama Hilda Ngai, anauguliwa na kaka yake, amelazwa ICU, Muhimbili, tumtembelee na kumuombea.
--  
16. Utaratibu wa Sabato ya leo—Tarehe 25.05.2013



 
TUKIO
TEGETA
WATOTO
Mhubiri
MWJ MALEMA
MAMA MAINGU JANDWA
Mwenyekiti
MZEE S.I.M. KAPAYA

Fungu Kuu na Ombi
MZEE B.I.MORRO

Sadaka & zaka
NDG ANANIA MNDEME

Kufunga Sabato
EFOTI AFYA


17. Utaratibu wa Sabato ijayo—Tarehe 01.06.2013

TUKIO
TEGETA
WATOTO
Mhubiri
MWJ MALEMA
MZEE JOSEPH MSUYA
Mwenyekiti
MZEE RICHARD BARIKESHA

Ombi na Fungu Kuu
ADAM MSAKU

Sadaka/Zaka
DAMBA OMARA

Maombi J5 (Jioni)
MAOMBI ECD/EFOTI

Maombi J5 (Asubuhi)
MAOMBI ECD/EFORI

Kufungua Sabato
MAOMBI ECD/EFOTI


18. Ratiba Fupi ya Mchungaji ni kama ifuatavyo:

MWEZI
TAREHE
SEHEMU HUSIKA
TUKIO

12
Madala
Baraza la kanisa
Mei
14-18
Mbweni
Uamsho

24-31
Boko
Uamsho  
Juni
01-08
Tegeta
Uamsho

09-16
Temeke
Kambi la uwakili

18-22
Kisanga
Uamsho

25-30
Bunju
Uamsho

19. Ratiba ya Mabaraza ya Uhai ya Kila Robo-II

KANISA HUSIKA
BARAZA LA KANISA
BARAZA LA MASHAURI YA KANISA
TAREHE
MUDA
TAREHE
MUDA
BOKO
23/6/2013
1.00-7.00
30/06/13
8.00-12.00
BUNJU
30/6/2013
1.00-7.00
07/07/13
1.00-7.00
KISANGA
19/5/2013
1.00-7.00
26/05/13
8.00-12.00
MADALA
09/6/2013
1.00-7.00
17/06/13
8.00-12.00
MBWENI
26/5/2013
1.00-7.00
02/06/13
8.00-12.00
TEGETA
16/6/2013
1.00-7.00
23/06/13
8.00-12.00
BARAZA-MTAA
02/6/2013
3.00-8.00
HAKUNA
HAKUNA


Ahsanteni na Mungu Awabariki!!

No comments

Powered by Blogger.